Wakati mwingine katika kazi, unaweza kujikuta uko njia panda. Kazi yako haikulipi vizuri lakini unaipenda sana. Je, unapaswa kufanya kazi ambayo unafurahia lakini haikulipi vizuri?
Vipi ikiwa utahitaji kuwa vizuri kifedha ili uweze kuanzisha biashara yako mwenyewe au uweze kuchukua familia yako kwenda likizo bila kuwa na wasiwasi kuhusu fedha?
Kwa wengine, fedha ni muhimu zaidi, lakini kwa wengine, kuridhika na kazi kunaweza kuwa kipaumbele cha juu. Utafiti unaonyesha kwamba wafanyakazi wengi wanaamini kuwa watafurahi kama kazi yao itaendana na maslahi yao binafsi, ikiwa ni pamoja na mshahara bora.
Mshahara Mzuri vs Furaha Kazini.
Kutumia muda mwingi kufanya kazi ambayo huipendi na inakufanya uhisi kutoridhika nayo inaweza kuwa na athari mbaya juu ya afya yako kwa jumla. Kufanya kazi katika mazingira ambayo hayaendani na wewe, maslahi au maadili yako inaweza kusababisha ukakosa ujasiri, ukawa na shida na wasiwasi. Utafiti unaonyesha kwamba, kufanya kazi kwa muda mrefu katika mazingira magumu pia kunaweza kusababisha matatizo ya msongo wa mawazo na mahusiano.
Kazi Unayoipenda Dhidi ya Pesa.
Unapofanya kazi ambayo inaendana na utu wako, nguvu na unavutiwa nayo, kuna uwezekano wa kuwa na furaha na ufanisi. Hii ni kwa sababu utaelewa kazi yako vizuri na kuwa utaweza kushiriki kikamilifu, hivyo kupata ujasiri zaidi katika kutekeleza kazi.
Kwa nini Kazi Unayoipenda Ni Bora Zaidi na Si Mshahara.
Kuchagua fedha juu ya kazi unayoipenda kunaweza kutegemea mambo kadhaa. Inaweza kuwa sababu za familia, uhuru wako wa kifedha, ndoto, nk.
Lakini unapaswa kuzingatia mambo mengine ambayo yana msingi zaidi ya mshahara wa juu. Unapotaka kuamua kipi uchague kati ya kazi inayolipa vizuri au kazi unayoipenda, anza kwa kufikiria yafuatayo:
1. Tafuta Njia ya Kipato cha Ziada
Ikiwa upo njiapanda ya kuchagua kuchukua kazi ambayo unaipenda wewe kuliko inayolipa vizuri, anza kwa kufikiria ikiwa unaweza kufanya kazi kwa muda wako ili kupata fedha za ziada.
Ukiona unaweza kufanya kazi kwa muda wa ziada ili kuongezea mshahara wa chini utakaopata, basi ni bora kuamua kufanya kazi ya ndoto zako.
2. Jipange Upya Kulingana na Bajeti Yako.
Hatua nyingine ya kuchukua ni kwamba, unapaswa kubadili maisha yako kidogo ili kuendana na kipato kidogo utakachokuwa unakipata katika kazi unayoipenda. Unaweza kuja na bajeti na uhakikishe gharama zako ili uone kile cha kupunguza kwa kipindi hiki cha mwanzo unachofurahia maisha ya kazi yako huku ukiendelea kukua pole pole.
3. Tanguliza Vipaumbele Kwanza.
Pia, unapaswa kuchunguza kazi ya ndoto zako ili kuhakikisha unajua wastani wa mshahara na matarajio ya kazi ya baadaye. Hii itakusaidia kuelewa nini unachoweza kufanya ikiwa unaendelea kufanya kazi katika taaluma iyo. Ikiwa kuna nafasi utaweza kupata mshahara wa kutosha kulingana na uzoefu wako, basi unapaswa kuendelea kufanya kazi unayoipenda kwani mbeleni utafanikiwa sana.
Mwisho, ikiwa itatokea uko katikati ya kuchagua kazi nzuri au kuchukua kazi unayopenda, fanya utafiti wako kwanza. Ingawa hakuna njia maalum ya kuhakikisha furaha yako, lakini kufanya kazi unayopenda ni njia sahihi ya kuchukua.