Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Singida inamshikilia Mshindi wa Kura za Maoni (CCM) Jimbo la Singida Kaskazini, (kabla ya kufutwa), Haider Gulamali kwa tuhuma za kutoa Rushwa.
Gulamali aliibuka kidedea kwenye mchakato wa kura ya maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi ili kusaka nafasi ya kumrithi aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Lazaro Nyalandu aliyetimkia CHADEMA.
Hata hivyo zoezi hilo lililoendeshwa kinyume na katiba limefutwa na katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na kurudiwa tena kwa taratibu zitakazotolewa na uongozi.
-
CCM yafuta mchakato kura za maoni Singida Kaskazini
-
Zitto, Bashe walaani kitendo cha Serikali kuuliza Uraia wa Askofu
Aidha wafuasi hao waliokamatwa kwa tuhuma za rushwa hawataruhusiwa tena kugombea nafasi hiyo ya Ubunge wa Singida Kaskazini kupitia tiketi ya Chama Chama cha Mapinduzi (CCM).