Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza amezindua kampeni ya kura ya maoni ambayo itapelekea kubadili Katiba ya nchi hiyo na kumfanya abakie madarakani hadi mwaka 2034.

Shirika la habari la AFP limesema kuwa mpango huo unahusisha kuidhinishwa kwa rasimu ya katiba ambayo itamuwezesha kuwania urais kwa mihula miwili zaidi ya miaka saba kila muhula.

Aidha, Rais huyo amewaambia wafuasi wake katika kijiji cha Gitega kuwa wale wanaopinga juhudi zake, kwa maneno au kwa vitendo watakuwa wameuvuka mstari mwekundu.

Kampeni hiyo imeanzishwa baada ya serikali kuzindua kampeni nyingine ya kuchangisha fedha za maandalizi ya uchaguzi mkuu wa urais unaotarajiwa kufanyika mwaka 2020.

Hata hivyo, Burundi ilitumbukia kwenye mgogoro wa kisiasa mwaka 2015, ambapo Rais Nkurunziza alipokataa kung’atuka baada ya kumaliza muhula wake.

Mshindi wa kura za maoni CCM atiwa mbaroni
Tanzia: Mtoto wa ''Mo'' Ibrahim apoteza maisha