Mbunge wa Iringa Mjini kupitia tiketi ya (CHADEMA), Peter Msigwa amewataka watu kutoleta masihara katika suala zima la matibabu ya Mbunge wa Singida Mshariki, Tundu Lissu kwani mbunge huyo anahitaji uangalizi wa hali ya juu.
Msigwa ameyasema hayo mara baada ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kusema kuwa serikali ipo tayari kulipia gharama za matibabu ya mbunge huyo mahali popote duniani baada ya kupata maombi kutoka kwa familia ya Tundu Lissu na kama ripoti ya madaktari itaonyesha kuna ulazima wa kiongozi huyo kupatiwa matibabu zaidi basi serikali itasimamia jambo hilo.
Msigwa amedai kuwa matamko ya baadhi ya watu yaanaleta kuwa masihara katika shughuli nzima ya matibabu ya Lissu huku wakishindwa kuelewa kuwa mbunge huyo anahitaji msaada wa haraka ili kuweza kurudi katika hali ya kawaida.
“Kuna watu wanaleta utani katika suala hili la matibabu ya Mheshimiwa Lissu, Mbunge huyu anahitaji msaada mkubwa katika matibabu yake lakini kuna baadhi ya watu wanaleta masihara,”amesema Msigwa
-
Mbunge wa CCM aliyemkodia ndege Lissu atoboa siri
-
Lema: Lissu bado yupo ICU
-
Kubenea augua ghafla Dodoma
-
Lissu ampa ujumbe mzito Zitto, ‘Tumeshinda
Hata hivyo, Msigwa ameongeza kuwa wao wanatambua thamani na umuhimu wa Tundu Lissu na kusema kuwa wapo tayari kuuza vitu vyao mbalimbali ili kuhakikisha kuwa kiongozi huyo anapata matibabu na kurejea nchini akiwa salama.