Rais Yoweri Museveni amesema hana wasiwasi kufuatia Uganda kuondolewa katika mpango maalumu wa kibiashara wa Marekani na Afrika – AGOA.

Kuondolewa kwa Uganda, kunafuatia Museveni kuikosoa Marekani akisema Taifa hilo linadhani nchi za kiafrika haziwezi kujiendeleza bila misaada kutoka nje.

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni. Picha ya Abubaker Lubowa/ REUTERS.

Aidha, Rais wa Marekani Joe Biden alisema nchi nyingine tatu za Afrika zitaondolewa katika umoja huo, akitaja sababu za kuondolewa huko kuwa ni ukiukuaji wa haki za binadamu unaotambulika kimataifa.

Museveni alisema, “tuna wezo wa kufikia malengo yetu ya ukuaji na mabadiliko bila hata kuungwa mkono, pengine Wahisani hudhani hatuwezi kujiendeleza wenyewe kitu abacho wanajidanganya.”

Serikali yapanga kutumia shilingi tilioni 47.424
Real Madrid yakanusha mpango wa Mbappe