Waziri wa Ardhi, Nyumba na Mendeleo ya Makazi Jerry Silaa amemuagiza Mthamini Mkuu wa Serikali na Kamishina wa Ardhi kufika Mbeya ndani ya siku mbili ili kutatua mgogoro wa Ardhi kati ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) katika eneo la Uyole na wakazi wa mtaa wa Sae na Ituha jijini Mbeya
Ameyasema hayo mara baada ya kufanya ziara katika eneo lenye mgogoro wa Taasisi hiyo na wakazi wa mtaa huo ambao wanadaiwa kuwa ni wavamizi wa eneo ili kuanza mchakato wa uthamini na ulipaji fidia.
Aidha Silaa ametoa siku hizo mbili kwa Mthamini Mkuu wa Serikali na Kamishina wa Ardhi kufika jijini Mbeya mara baada ya kusikiliza kwa makini maelezo ya mgogoro huo na kutaka kuharakisha utoaji maamuzi ya mgogoro huo.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya TARI Dkt Geofrey Mkamia ameeleza namna TARI ilivyojitahidi kushirikisha wakazi hao katika kutatua tatizo hilo bila mafanikio.
Aidha ameeleza umuhimu wa eneo hilo lenye faida kwa Taifa.