Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani kikwete amesikitishwa na wimbi kubwa la wafanyakazi hasa walimu kutuma maombi ya kutaka kuhama katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, Mkoani Iringa.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Kilolo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi mkoani humo ya kuzungumza na kusikiliza kero za watumishi na kuzitafutia ufumbuzi.

Kikwete amesema watumishi waliowengi wanaotaka kuhama wamekuwa wakitaja sababu zinazofanana jambo ambalo linawalakini huku akisema kuna matatizo ya kiuongozi katika Halamshauri hiyo ambapo ametaja moja ya sababu ambapo ametaja moja ya sababu zinazopelekea watumishi kutaka kuhama ni pamoja na kuupuzwa.

”Kuna watumishi hapa hawajapandishwa vyeo kwa muda wa miaka 9 na wengine licha ya kujiendeleza kielemu mishahara yao haijabadilika lakii ninyi maafisa utumishi wenye jukumu la kufuatilia na kuwapa majibu mpo tu hii si sawa hata kidogo Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala mmkuwa miungu watu badala ya kuwa suluhusho la matatizo yanayowakabili watumishi mmnao wasimamia”

Amesema licha ya sababu kuu ya watumishi wengi kutaka kuhama kuwa ni baridi kali na hivyo kusumbuliwa na ‘athma’ jambo amabalo si kweli ukweli ni kwamba hakuna mahusiano mazuri kati ya watumishi na Uongozi wa Halmashauri

Naibu waziri Kikwete amemtaka Mkurugenzi kufanyia kazi changamoto zinawakabili watumishi hao ikiwemo ikiwemo kufanya vikao vya mara kwa mara kwa ajili ya kuwasikiliza pamoja na kuzingatia stahili zao ikiwemo posho za likizo.

Mthamini Mkuu, Kamishina wa Ardhi wapewa siku mbili
Wakandarasi wababaishaji hapa mwiko- Bashungwa