Shirika linalojihusisha na Ulemavu kwa Vijana nchini -YOWDO, limezindua tovuti maalumu ijulikanayo kama -YOWDO Connect Portal, itakayowakutanisha
kwa pamoja Vijana wenye Ulemavu na waajiri kwa lengo la kusaidia vijana hao kuweka taarifa zao muhimu ikiwemo wasifu na aina ya ulemavu, ili kuwasaidia kupata ajira.

Akizungumza katika uzinduzi wa tovuti hiyo hii leo Novemba 24, 2023 kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni mgeni Rasmi na Afisa Afya Wilaya ya Kinondoni, Kijumbe John amesema tovuti hiyo itasaidia wazazi kuwasomesha watoto wao wenye ulemavu bila kuwaficha.

Amesema, “hii itatoa nafasi kwa wazazi ambao walikuwa wanafikiria kwamba nikimsomesha mwanangu atapata wapi ajira hivyo mtoto akisoma ipo sehemu ya kujitangaza kupitia elimu yake na kupata fursa ya kupata ajira.”

Aidha, kijumbe amesema “Tovuti hii inawawezesha waajiri kujua muombaji wa kazi anakipaji gani, elimu ipi na aina yake ya ulemavu ni kitu kizuri hii ni fursa kubwa
ifikie wakati wenzetu wenye ulemavu wajione sasa wamepata mkombozi.”

Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa linalojihusisha na Watu wenye Ulemavu -Adot, Rose Choma amesema uzinduzi wa tovuti hiyo utasaidia pande zote mbili kwa muajiri na muajiriwa, kufahamu taarifa zote za mlemavu, kuweka wasifu wake na kupata fursa kwa muajiri kufahamu na
kupata muda wa kuandaa mazingira wezeshi ya kumsaidia muajiriwa wake kupata kazi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa – YOWDO, Emanuel Mkude amemshukuru mgeni rasmi na kusema wanachokifanya ni kutekeleza haki na sharia hususan kwa vijana wenye ulemavu ili iwe njia rahisi ya kufungua fursa za ajira.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Novemba 25, 2023
Mthamini Mkuu, Kamishina wa Ardhi wapewa siku mbili