Waandaaji wa tuzo za MTV Europe Music Awards (MTV EMA 2016) wamekubali kuwa tuzo ya Best African Act waliyompa Wizkid ilitolewa kimakosa na kwamba Ali Kiba ndiye alistahili kupewa.

Jana, Ali Kiba alieleza kushangazwa kwake na utoaji wa tuzo hiyo kwani yeye ndiye aliyeongoza kwa kura zilizopigwa wazi kwenye mtandao.

Menejimenti ya Ali Kiba imeuambia mtandao wa Millardayo kuwa wamepokea taarifa kutoka kwa MTV EMA kuwa wamebaini makosa yaliyotokea hivyo Ali Kiba atapewa tuzo hiyo itakayotolewa mikononi mwa msani huyo wa Nigeria.

Wameeleza kuwa tayari wamewasiliana na Wizkid kuhusu mabadiliko hayo. Wizkid amefuta picha za tuzo hiyo alizokuwa amepost kwenye mitandao ya kijamii.

Juan Antonio Pizzi: Sanchez Atacheza Dhidi Ya Man Utd
Video: Machinga watakiwa wasiishi kwa mazoea