Baraza la Madiwani Manispaa ya Ilala leo Novemba 9, 2016 limekutana kwa ajili ya kuangalia jinsi gani ya kuweza kutatua matatizo mbalimbali ya ujenzi holela na wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama Machinga.

Hayo yamesemwa na Kassim Mshamu, Diwani wa kata ya miti mirefu na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Mipango Miji na Mazingira alipokuwa akizungumza na waaandishi wa habari mapema leo, ameongeza kuwa  kuna tatizo kubwa la Machinga katika Manispaa ya Ilala ingawa si wote wanaoishi Ilala bali wengi wao wanatokea sehemu mbalimbali za jiji, hivyo amezitaka Halmashauli nyingine kutengeneza utaratibu kwa ajili ya Machinga.

Aidha ameongeza kuwa wana mpango wa kuiweka Ilala katika hali ya usafi ikwa ni mwendelezo wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli la kufanya usafi kila siku za jumamosi na kila mwisho wa mwezi.

MTV EMA Wakiri tuzo waliyompa Wizkid ni ya Ali Kiba, wampokonya
Majaliwa apokea msaada kutoa kwa Balozi wa Kuwait