Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe ameagiza kuanza upya kwa zoezi la usajili wa daftari la wapiga kura wakati nchi hiyo ikijiandaa na uchaguzi mkuu wa kiti cha urais na wabunge mwaka ujao.
Katika agizo hilo la Rais huyo wa Zimbabwe ametoa miezi minne ya kujiandikisha upya katika daftari la wapiga kura ili kuweza kuepukana na usumbufu wowote ambao unaweza kujitokeza wakati wa zoezi la upigaji kura hapo mwakani.
Aidha, Zimbabwe inatarajia kufanya uchaguzi huo mwaka ujao kwa kutumia daftari hilo jipya la usajili wa wapiga kura ikiwa ni moja ya mabadiliko ambayo Rais Mugabe ameamua kuyafanya baada ya vyama vya upinzani kupigia kelele suala hilo.
-
Jaji Lubuva akerwa na kauli za wanasiasa
-
Video: Madereva wengi wanadharau- Kamanda Msangi
-
Video: Hii ni laana na unyama kuhujumu uchumi wa nchi- Dkt. Mpango
Hata hivyo, mwaka 2008 vyama vya upinzani nchini humo vilisema kuwa vimegundua makosa ikiwemo kusajiliwa kwa wapiga kura wengi waliokuwa hawaeleweki walipokuwa wakiishi hivyo kusababisha malalamiko mengi kutokea.