Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe amesema kuwa hamuungi mkono mrithi wake Rais wa sasa Emmerson Mnangagwa ndani ya chama tawala Zanu PF, kwa kile alichodai kuondolewa kwa nguvu madarakani na chama alichokianzisha.

Ametoa kauli hiyo wakati wa mkutano wake na wanahabari Jijini Harare, ikiwa zimesalia saa kadhaa kabla ya taifa hilo la kusini mwa Afrika kufanya uchaguzi mkuu hapo kesho.

Aidha, amesisitiza kuwa, hawezi kuwapigia kura watu waliomtesa na kwamba kura yake atampigia mmoja kati ya wagombea wengine 22 wanaowania nafasi ya urais.

“Namtakia kila kheri kiongozi wa chama cha upinzani cha Vuguvugu la Mageuzi ya Kidemokrasia, MDC, Nelson Chamisa katika uchaguzi wa kesho. Kijana huyu ndio anaonekana kufanya vizuri na ndiye mgombea anayefaa,”amesema Mugabe

Hata hivyo, zaidi ya raia milioni tano wa Zimbabwe wanajiandaa kumchagua Rais kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 38 bila Mugabe madarakani.

 

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Julai 30, 2018
Video: Haji Manara afunguka kuhusu Jerry Muro kuteuliwa Ukuu wa Wilaya