Mwanamke mmoja nchini Kenya aliyechoshwa na tabia ya mumewe ya kulewa kila siku na kuamua kumfuata baa na kuanza kumhubiria pamoja na walevi wengine waliokuwepo kwenye baa hiyo juu ya kuacha kutumia pombe.

Tukio hilo limetokea katika mtaa wa Embakasi, Nairobi ambapo mwanamke  huyo aliingia kwenye baa na kuanza kumhubiria mumewe.

Inadaiwa kuwa mama huyo alikuwa amechoshwa na tabia ya mumewe na ndipo alipoamua kuchukua hatua hiyo.

Inasemekana kuwa mahubiri yake yalikuwa mazito na hata kuwavutia baadhi ya wanaume waliokuwa wakistarehe kwa mvinyo katika baa hiyo na kupelekea kuacha kubugia pombe ili kumpa sikio mama huyo aliyekuwa na biblia mkononi.

Kulingana na mdokezi, baadhi ya walevi hao waliacha kunywa pombe na kukubali kuokoka.

’ Baadaye, baadhi yao waliokoka na wengine wakaacha pombe mezani kurudi makwao. Hii haikuwafurahisha wasimamizi wa baa lakini hawakuweza kumfukuza baada ya kutetewa vikali na wateja waliokuwa wakimsikiliza,’’ alisema.

Aidha, Inadaiwa kuwa mumewe mwanamke huyo aliondoka kwenye baa hiyo na kuahidi kutokunywa pombe tena.

Waitara ang'oka Chadema, adai Mbowe ni tatizo
Mkurugenzi Mkuu CBS achunguzwa kwa kashfa ya ngono