Aliyekua Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe amevunja ukimya kwa mara ya kwanza tangu aondolewe Madarakani kwa kusema kuwa yeye ni muhanga wa mapinduzi ya kijeshi.
Akiongea na televisheni ya SABC ya Afrika kusini Mugabe amesema kuwa Rais wa sasa, Emerson Mnangagwa asingeweza kuingia madarakani bila kutumika kwa jeshi.
Aidha, amesema kuwa alikua tayari kufanya mazungumzo na Rais wa sasa Emerson mnangagwa na angehakikisha mabadiliko ya madaraka ya uhalali na si yale ya kulazimishwa.
“Siamini kama yeye Mnangagwa angeweza kuniondoa madaraki , nimemuingiza serikalini, nimemsaidia alipokua jela anataka kunyongwa, sikuwaza kabisa kama siku moja yeye ndio atakua mtu wa kunitoa madarakani,”amesema Mugabe
Hata hivvo, Mugabe amesema kuwa kuko tayari kwa ajili ya Mazugumzo na Mnangagwa ili kulinda katiba yao kwa ajili ya maendeleo ya nchi yao.