Muuguzi wa Hospitali ya Taifa nchini Kenya amekiri kufanya kosa la kumpeleka mgonjwa asiyehitaji upasuaji katika chumba cha upasuaji.

Amesema kuwa aligundua kosa lake baada ya madaktari kufanya upasuaji na kusema hawakuona uvimbe kwenye ubongo wa mgonjwa huyo.

Madaktari wa hospitali ya taifa ya Kenyatta jijini Nairobi walitakiwa kumpasua mgonjwa aliyekuwa na mgando wa damu kwenye ubongo lakini aliyepasuliwa hakuwa anahitaji huduma hiyo.

Hata hivyo, tukio hilo lilipelekea wafanyakazi wanne kufukuzwa kwa muda wakiwemo madaktari wa upasuaji wa ubongo, muuguzi aliyekuwa akisimamia wodi, na afisa wa kuwatia ganzi wagonjwa.

Wadau wa elimu Rukwa watoa maoni kwa tamko la Rais
Mugabe: Sikutegemea kama nitang'olewa madarakani