Tetesi za usajiliwa Kiungo wa Gor Mahia na timu ya Taifa ya Kenya, Kenneth Muguna, kutakiwa na mabingwa wa kihistoria Young Africans, zinaendelea kushika kasi baada ya mtandao wa Goal.com kubaini hilo jana Jumanne jioni.

Taarifa zinaeleza kuwa kiungo huyo fundi atamaliza mkataba wake Julai 30, hivyo atakuwa huru kujiunga na klabu yoyote.

Young Africans inasaka mbadala wa kiungo mkongwe Haruna Niyonzima ambaye nafasi yake imeendelea kuwa finyu kwenye kikosi cha Kocha Nasrideen Nabi.

Muguna amekuwa mchezaji muhimu wa Gor Mahia na timu ya Taifa ya Kenya juzi akiisaidia Gor Mahia kupata ushindi wa mikwaju ya penati 4-1 dhidi ya AFC Leopards katika mchezo wa fainali ya kombe la FKF.

Awali Young Africans ilikuwa ikihusishwa kumuwania kiungo wa DR Congo Merceil Ngimbi Vumbi, ambaye amejiunga na TP Mazembe.

Ambani atoa ushauri kwa Shikalo
Young Africans yampotezea Kibu Denis