Rais Yoweri Museveni amesema Magaidi wamejidhihirisha kipindi ambacho miundombinu ya usalama ya Nchini humo imeimarika, ikilinganishwa na awali
Rais Museven amesema magaidi waliojilipua karibu na Kituo Kikuu cha Polisi (CPS) Mjini Kampala na karibu na eneo la Bunge ni “Bazzukulu” (inayomaanisha Wajukuu) waliodanganywa na kuchanganyikiwa
Museveni amemtambulisha mshambuliaji wa kujitolea mhanga kufa katika kituo cha polisi cha Central kuwa Mansoor Uthman na mwenzake aliyejilipua kwenye barabara ya Parliament Avenue kuwa Wanjusi Abdallah.
Wakati huo huo kundi la Islamic State limesema lilihusika kwenye milipuko miwili iliyotokea siku ya Jumanne mjini Kampala.
Raia watatu, na washambuliaji watatu wa kujitolea mhanga kufa waliaga dunia kwenye mashambulizi hayo, huku watu wengine zaidi ya 30 wakijeruhiwa.
Hii ni mara ya tatu ambapo kundi la Islamic State limedai kuhusika kwenye mashambulizi nchini Uganda tangu mwezi Oktoba mwaka huu