Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amesema kuna umuhimu kwa mataifa yalioendelea kutoa msaada wa haraka katika mapambano dhidi ya UVIKO – 19 pamoja na ufufuaji uchumi kwa mataifa yanayoendelea hasa Kusini mwa Jangwa la Sahara.
 
Ameyasema hayo wakati wa Mkutano wa Jukwaa la Majadiliano ya Kiuchumi, katika kisiwa cha Sentosa nchini Singapore ambapo mkutano unaojadili masuala mbalimbali ikiwemo muelekeo mpya wa kiuchumi baada ya athari za UVIKO – 19 pamoja na mabadiliko ya Tabianchi.

Amesema katika mapambano dhidi ya UVIKO – 19, nchi za Afrika ikiwemo Tanzania zimepitia changamoto kubwa ikiwamo kuelemewa kwa mfumo wa utoaji huduma za afya kutokana na kutokuwepo kwa miundombinu na vifaa vya kutosha kupambana na ugonjwa huo.
 
Kwa mujibu wa Dkt. Mpango, ugonjwa wa UVIKO – 19 umeacha madhara kwa familia kupoteza wapendwa wao waliowategemea, hivyo kuziingiza familia nyingi katika umaskini jambo linalotakiwa kuangaliwa kwa umuhimu mkubwa.

Museveni awataja waliojilipua Uganda
Kesi ya Mbowe na wenzake yaahirishwa mara tatu