Baada ya kukwama kwa usafiri wa meli tangu mwaka 2014 kati ya Bukoba na Mwanza meli ya MV New Victoria hapa kazi tu kuanza safari zake tena ifikapo Agosti 16, 2020 kupitia bandari ya Kemondo na Ukerewe Mkoani Mwanza.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Meli Tanzania MSCL amesema kutakuwa na nauli tofauti kulingana na madaraja yaliyopo, daraja la kawaida shilingi 16,000, Daraja la pili lenye vitanda vinne vya kulala shilingi 30,000, na watakao safiri daraja la kwanza watalipa shilingi 45,000.
“Muda wote wa safari abiria watapata huduma ya chakula na vinywaji katika migahawa na baa zilizopo katika madaraja yote” Amesema Hamisi
Aidha amesema safari zinaanza baada ya kupatikana kwa vibali na vyeti vya ubora kutoka shirika la uwakala wa meli (TASAC) pamoja na meli hiyo kuanza safari zake meli nyingine inayotarajiwa kuanza safari ni MV Butiama.
Pamoja na meli hizo kuanza kufanya kazi pia serikali inajenga chelezo kuunda meli mpya ya Mv Mwanza miradi yote inagharimu kiasi cha sh 152 bilioni, ikumbukwe
Ikumbukwe Meli ya MV Victoria ambayo sasa inaitwa Mv New Victoria iliundwa mwaka 1965 na kusitisha huduma 2014 kutokana na uchakavu imegharimu zaidi ya sh 4.9 bilioni na inabeba abiria 1,200 na tani 200 za mizigo.