Jeshi la Polisi Nchini, limewatahadhari Wananchi juu ya mvua zinazoendela kunyesha huku likisema linao wajibu wa kulinda maisha ya watu na mali zao, ambapo limetoa tahadhari kwa Wananchi wote kuhusiana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali hapa Nchini.
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, David Misime amesema tayari wamepokea taarifa mbalimbali za watu wazima na watoto kufa maji wakati wakijaribu kuvuka mito na barabara zilizojaa maji na wengine wakiogelea kwenye mashimo, madibwi Pamoja na mabwawa yaliyojaa maji ya mvua.
Amewataka Wananchi kuchukua tahadhari kubwa wanapotaka kuvuka mito,madaraja,makorongo ambayo yamejazwa na mvua zinazoendelea kunyesha ambapo ameongeza kuwa mvua zinazoendelea kunyesha hazina urafiki na yeyote anayetakakushindana nazo.
Aidha, amewaomba wazazi na walezi kuongeza ungalizi Mkubwa kwa watoto kipindi hiki cha mvua ambazo zimetabiriwa kuendelea kunyesha maeneo mbalimbali ya nchi ambapo amewataka wazazi kuwaonya na kutowaruhusu kwenda kucheza au kuogelea kwenye mito,makorongo yanayopitasha maji ya mvua Pamoja na madimbwi mabwawa.
Misime pia amewasihi Wananchi wote ambao wamechimba mashimo na kuyaacha wazi wayafukie ili yasihatarishe Maisha ya watu, huku akitoa wito kwa Viongozi wa Serikali za Mitaa kuendelea kushirikiana na Polisi Kata, kutoa elimu na tahadhari kwa wananchi ili kuwaepusha madhara ya mvua zinazoendelea kunyesha.