Wakati bondia, Suleiman Kidunda akimuondoa Dullah Mbabe kwenye reli ya ubora, Twaha Kiduku na Hassan Mwakinyo kila mmoja anapita njia yake kuhakikisha anakuwa bora kwenye renki.
Kwa mujibu wa Mtandao wa ngumi za kulipwa wa dunia (Boxrec), mabondia hao nyota nchini kila mmoja anapambana kusalia kwenye ubora, japo kudunia bado hali si shwari kwa Mwakinyo.
Mwakinyo ameporomoka kwa mara ya pili tangu azichape na Liam Smith Septemba 3 nchini Uingereza.
Kabla ya pambano hilo, alikuwa kwenye nafasi ya 37, baada ya pambano aliporomoka hadi nafasi ya 39 na karibuni ametajwa kuwa wa 41 kwenye uzani wa super welter.
Hata hivyo hapa nchini ameendelea kuwa kinara kwenye uzani huo, lakini pia kwenye kila uzani (pound for pound) ambako nafasi ya pili inashikiliwa na Tony Rashid na Ibrahim Class ni wa tatu.
Kiduku kwenye pound for pound ameendelea kung’ang’ania nafasi ya tano, wakati kwenye uzani wake wa super middle akiwa kinara.
Dullah Mbabe ambaye jina lake halisi ni Abdallah Pazi ameporomoka kwenye uzani huo, akimpisha Kidunda kwenye nafasi ya pili aliyokuwa akiishikilia kwa zaidi ya miaka minne na sasa ni wa tatu.
Kidunda ambaye kwenye pound for pound anakamata nafasi ya 10, kwenye uzani wa super middle ni wa pili nchini, nyuma ya Kiduku.
Kwenye pound for pound walioingia 10 bora ni Mwakinyo, Tony Rashid, Ibrahim Class
Mgender, Juma Choki, Kiduku, Said Chino, Ismail Galiatano, Fadhili Majiha, Muksini Swalehe ne Selemani Kidunda.
Chanzo: Mwanaspoti