Mwanamuziki maarufu nchini, Adolph Mbinga amefariki dunia usiku wa kuamkia June 16, 2023 katika Kijiji cha Mpute, kilichopo Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi.

Mbinga kwa siku za hivi karibuni, alikuwa na matatizo ya kiafya akijiuguza nyumbani kwake Kitonga jijini Dar es Salaam kabla ya kwenda kwao Mkoani Lindi.

Enzi za hai wake, Mbinga aliwahi kuhudumu bendi kadhaa zikiwemo Diamond Sound, Twanga Pepeta, Mchinga Sound, Sikinde na Sikinde OG.

‘Mtuhumiwa’ Adolf Mbinga – ‘Chinga One’, enzi za uhai wake.

Alianza kazi zake za muziki wa dansi akiwa Mkoani Lindi mahali alipozaliwa, na alijulikana zaidi kwenye miaka ya 2000 akiwa na bendi ya African Stars “Twanga Pepeta” kufuatia utunzi wa kibao chake cha Kisa cha Mpemba, kilichovuma nchini.

Baadaye, alijiunga na bendi ya Mchinga Sound ambayo ilikuwa inamilikiwa na Mohamed Mudhihir, huku akipata umaarufu mkubwa kwa kushirikiana na akina Muumin Mwinjuma, Joseph Watuguru, Roshi Mselela, Seleman Bongo, Deo Mwanambilimbi na Michael Liloko.

Mabadiliko tabianchi: Wananchi washiriki upandaji miti - Jafo
Simba SC kumshusha Bongo Makabi Lilepo