Malkia wa muziki wa rock Tina Turner afariki dunia akiwa na umri wa miaka 83 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Mashabiki wa muziki duniani kote wanaomboleza kuaga dunia kwa gwiji huyo ambaye alifanikiwa kuvuma kwa kiasi kikubwa na habari zake kuenea kwa vizazi na vizazi. Tukio hili la kusikitisha linajiri miezi michache tu baada ya kufiwa na mwanawe mpendwa Ronnie Turner.

Turner alijitokeza hadharani kuweka wazi kuhusu masuala kadhaa ya afya ambayo yaliyokua yakimkabili katika miaka ya hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na kiharusi, saratani ya tumbo, shinikizo la damu na kushindwa kufanya kazi kwa figo.

Turner aliwateka wengi alipokuwa stejini akitumbuiza, sauti yake nzuri na safari yake ya muziki hakika imeacha alama isiyoweza kufutika kwenye tasnia ya muziki na mioyo ya mamilioni ya watu walioufuatilia muziki wake ulimwenguni kote.

Turner alifanikiwa kufanya vyema na nyimbo nyingi ikiwamo “Simply the Best”, “What’s Love Got to Do with It” pamoja na nyingine nyingi zilizompa sifa kubwa na kumuwezesha kupata tuzo nyingi za Grammy, kutambuliwa kwa heshima na kituo cha Kennedy mnamo mwaka 2005 na hata kuingia kwenye jumba la maarufu la Rock and Roll mnamo mwaka 1991.

Young Africans yamshitaki Fei Toto kamati ya nidhamu
Ibenge: Young Africans itatwaa Ubingwa Afrika