Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ Mwita Kichere amejitokeza hadharani na kumjibu Haji Manara, baada ya kuzungumza na Waandishi wa Habari juzi Jumatatu (Julai 25) na kudai alidhalilishwa kupitia taarifa ya hukumu yake iliyosomwa Jumatano (Julai 21).
Manara alidai taarifa ya hukumu iliainisha alikuwa na Sigara na Kibiriti cha Gesi wakati wa mchezo wa Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ jijini Arusha, jambo ambalo alisisitiza liliainishwa kwenye hukumu hiyo kwa lengo la kumdhalilisha.
Mwenyekiti Mwita Kichere amesema hata yeye alikuwa na Sigara akiwa makao makuu ya TFF akisoma hukumu.
Akiongea na Efm Radio amesema, yeye hiyo ni style yake tuu lakini huwa haiwashi Sigara anayoishika.
Baada ya kuongea na waandishi wa habari Manara aliandika katika ukurasa wa mtandao wa kijamii: “Kamati ya Maadili ya (TFF) wakati inakwenda kusoma hukumu yangu iliyojaa dhulma,, Ilisema eti nilikwenda uwanjani na pakti ya Embassy na kiberiti cha Gesi, ambavyo mpaka sasa hatujui kwa nini waliamua kuongea vile na vina uhusiano gani na shauri langu”
“Sasa mwenyekiti wa hiyo kamati iliyosoma hukumu yangu, akiwa ndani ya ofisi za Shirikisho,, Tena akiwa anaongea na Wanahabari katika moja ya mikutano yake, aliingia huku anavuta shisha,, Aaahh sory ni Cigar”
“Imagine mnanituhumu mimi kuja na pakti ya Embassy huku nyie mbele ya Camera za media, mnakwenda na misigara mikubwa mikubwa ambayo hata hatujui ni tumbaku za aina gani zimo ndani yake”
“Maadili ya wapi hayo au ni haji tu na Embassy zake za uongo uongo !”
“Ok ndio wakubwa wetu hao wanaotuongozea vyombo vyetu vya kimaadili”