Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka wananchi wa Jimbo lake kutoulizia Milioni 50 za kila kijiji ambazo ziliahidiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema kuwa Serikali imetoa milioni 800 kwa ajili ya kujenga hospitali za Tarafa katika baadhi ya Kata kwenye jimbo hilo pamoja kupatiwa bilioni 2 kwa ajili utekelezaji miradi ambayo itawanufaisha wananchi wote.
“Nisikilizeni wana Iramba, Serikali imetupatia milioni 800 za kujenga hospitali za Tarafa Kinampanda na Ndago, tumepata zaidi ya bilioni 2 kujenga daraja tarafa ya Shelui, tumeshapata zaidi ya bilioni 2 kwa ajili ya maji.
Aidha, Nchemba amesema kuwa hizo ni huduma za watu wote na hazikuwepo kwenye ilani, ambapo ni upendo na maono ya Rais. Dkt. Magufuli hivyo wanapaswa kushukuru.
-
Video: Kauli ya Bashiru yagonga vichwa, Waliokusanya kodi ‘kiduchu’ matatani
-
Aweso awatangazia kiama watakao tafuna fedha za mradi
-
Waziri Kamwelwe awatimua Wachina wawili nchini
Hata hivyo, ameongeza kuwa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kupitia ilani ya Chama Cha Mapinduzi aliahidi kutoa milioni 50 kwa kila kijiji kwa nchini kwa ajili ya maendeleo.