Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO, limezindua mwongozo wa kwanza wa kutafiti ugonjwa wa shida ya akili, unaoambatana na kushindwa kufikiri na kusahau, ikiwa ni njia mojawapo ya kuleta uelewa, kuzuia na kutibu magonjwa ya msingi ambayo husababisha shida ya akili.
Kwa mujibu wa WHO, ugonjwa huo wa kusahau na kushindwa kufikiria ambao watu wengi huita ni kichaa, ni moja ya changamoto kuu za kiafya katika kizazi cha sasa na ni sababu ya saba ya vifo duniani, huku utafiti wa ugonjwa huo ukichukua asilimia 1.5 pekee ya tafiti zote za kiafya.
Mwanasayansi Mkuu wa WHO, Dkt. Soumya Swaminathan anasema tafiti chache katika eneo hili la afya linarudisha nyuma mpango wa dunia wa afya ya umma wa afya ya akili unaotekelezwa kwa kipindi cha mwaka 2017 mpaka 2025 na ameongeza kuwa, “kushughulikia shida ya akili kunahitaji kufanyika utafiti na uvumbuzi ili kupata majibu kuweza kupatikana.
WHO, imetoa mwongozo huo kwa kuwalenga watunda será, wafadhili, jumuiya za watafiti wa magonja ya shida ya akili iki kuwezesha utafiti kuwa fanisi zaidi, wenye usawa na pale utakapo fanyika kuleta matokeo na mwongozo huo umetoa maeneo manne muhimu ya kufanyia utafiti ikiwa ni pamoja na kuangalia uzoefu wa tafiti nyingine za magonjwa ya kuambukiza, maendeleo ya sayansi na teknolojia bila kusahau akili bandia.
“Tunaweza kufikia maendeleo katika utafiti wa ugonjwa wa shida ya akili kwa kuimarisha na kufuatilia vichochezi vya utafiti vilivyoangaziwa katika mwongozo ili ili kusaidia kufanya ni kawaida nzuri utafiti.” Amesema Dkt. Ren Minghui, Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa WHO kwenye Magonjwa Yanayoambukiza na Yasiyoambukiza.
Hata hivyo, WHO imeahidi pia kuendelea kufanya kazi na wadau wote katika sekta husika ili kuhakikisha kwamba hatua zilizoainishwa katika mwongozo huo zinatekelezwa, hatua muhimu zinafikiwa, na malengo ya kimkakati yanatimizwa, kwa lengo kuu la kuboresha ubora wa maisha na msaada unaotolewa kwa watu wanaoishi na shida ya akili.