Uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, kuhusu tukio la Katibu wa Kanisa la Feel Free kujiua kwa kujinyonga, umeonesha kuwa marehemu, pamoja na mke wa Mchungaji wa Kansas Hilo Emmanuel Mgaya (Masanja), hawakuwa na  mahusiano ya kimapenzi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne ameyasema hiyo hii leo Oktoba 4, 2022 wakati akieleza uchunguzi juu ya tukio hilo lililoibua utata an hisia tkwa wananchi.

Amesema, “Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa mawasiliano ya huyo marehemu akiwa anaomba mahusiano ya kimapenzi na mtu ambaye inadaiwa ni mke wa Masanja.

Emmanuel Mgaya (Masanja Mkandamizaji), akiwa na mkewe.

Kamanda Muliro ameongeza kuwa, “Pia kabla ya tukio mke wa Masanja akiwa na mama mwingine walikwenda nyumbani kwa Marehemu kumueleza kwamba hataki jumbe za namna ile na hataki mahusiano na yeye.”

“Alifadhaika baada ya kuelezwa waziwazi kwamba yule ni mke wa mtu na hataki mahusiano nae, sasa mtitiriko wa visa hivyo unatoa nafasi ya kutokuwa na shaka na mazingira ya kifo kile,” alisema Muliro.

Aidha, Kamanda Muliro alibainisha kuwa, “Bila shaka atakua amejinyonga kwa sababu mbalimbali za fikra zake au sababu nyingine yoyote lakini hata hivyo bado Jeshi la Polisi haliwezi likaishia kwenye ushahidi wa awali ambao umeonekana…. mwisho huwa ni kufanya uchunguzi wa kitaalamu.”

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Octoba 05, 2022
Wito kuungana na ‘mama’ kutangaza vivutio vya Utalii