Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari amesema kuwa anasubiri ushahidi mwingine kutoka Arusha ingawa anahofia usalama wake mara baada ya jana kuwasilisha ushahidi huo Takukuru kuhusu madai ya kupewa rushwa kwa madiwani wawili wa Chadema wa Arusha mjini ili wahamie CCM.
Ameyasema hayo mara baada ya kuwasilisha vielelezo vingine vya ushahidi Makao Makuu ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), jijini Dar es Salaam, ambapo amedai kuwa usalama wa maisha yake uko hatarini kutokana na kupokea taarifa za vitisho kutoka kwa watu wasiojulikana.
Aidha Mbunge huyo amesema anatarajia kutoa taarifa polisi pamoja na kuwasilisha ushahidi wake siku yoyote atakayoona inafaa baada ya kuupokea kutoka mkoani Arusha.
“Nimefungua jalada, tumefanya mahojiano, na nimewakabidhi ushahidi. Ushahidi nilionao ni mkubwa mno umehusisha viongozi wengi, nami nimetoa kila nilichonacho na kuna nyaraka nyingine zipo Arusha zikifika kwa wakati muafaka nitaziwasilisha. Maelezo yangu mengine nimewaachia wao waendelee na uchunguzi,”amesema Nassari
-
IGP Sirro amtumia ujumbe dereva wa Lissu, ‘inanipa tabu’
-
IGP Sirro awaomba wananchi kusaidia kumpata aliyemtishia Nape kwa bastola
-
Video: RC Makonda awatembelea wagonjwa wa macho
Hata hivyo Nassari hivi karibuni alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema maisha yake yapo hatarini kiasi cha kufikia kuogopa hata kulala na simu zake kwa kuhofia usalama wa maisha yake baada ya kuweka tuhuma za viongozi wa Serikali wakitoa rushwa kushawishi madiwani wa Chadema kuhamia CCM.