Nchi ya Zimbabwe na mataifa mengine 14 ya Afrika, ni miongoni mwa mataifa 32 wanachama wa Umoja wa Mataifa ambayo yamejiepusha kupiga kura juu ya azimio la Baraza Kuu, la kutaka Urusi iondoe wanajeshi wake kutoka Ukraine.

Azimio hilo, ambalo kura yake ilifanyika usiku wa kuamkia Februari 24, 2023 ambayo ni mwaka mmoja wa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine wa Februari 24 mwaka jana, liliitaka Moscow kuondoa wanajeshi wake katika nchi hiyo.

Ubao wa matokeo ya upigaji huo wa kura. Picha ya ABC News.

Mbali na Zimbabwe, nchi nyingine za Afrika ambazo hazikupiga kura ni Algeria, Angola, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kongo, Ethiopia, Gabon, Guinea, Msumbiji, Namibia, Afrika Kusini, Sudan, Togo na Uganda.

Hata hivyo, nchi za Misri, Ghana, Ivory Coast, Kenya na Nigeria zilipiga kura kuunga mkono azimio hilo, huku Eritrea na Mali zikiipinga hoja hiyo na lilipitishwa baada ya nchi 141 kati ya 180 kuunga mkono hoja zilizowasilishwa.

PICHA: Viongozi Simba SC wateta na wachezaji
Mgombea auawa, uchaguzi wasimamishwa