Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, amesema kuwa hana taarifa za kujiuzulu kwa mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu na wala hiyo barua bado haijamfikia, na kuita kitendo alichokifanya ni umbea

Ameyasema hayo hii leo, ambapo amesema kuwa, Lazaro hakupaswa kutangaza hivyo kabla ya kuhakikisha barua imemfikia, hivyo kusema kuwa yeye kama spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hajapata taarifa za Mbunge huyo kujiuzulu.

Aidha, Pamoja na hayo Spika Ndugai amewataka wabunge wengine kuacha kuwashwa washwa na kufanya mambo ambayo ameyaita ni ya umbea, hivyo amewataka kuzingatia sheria na taratibu za kibunge.

 

Hakuna ndoa kati ya Dogo janja na Irene Uwoya?
Video: CCM yamlipua Nyalandu, JPM atangaza kiama kwa wakuu wa mikoa...