Kamati ya mazishi ya marehemu Agness Gerard maarufu kama Masogange iliyoundwa na wasanii wa filamu nchini imekubaliana michango ya rambirambi ilyobaki mara baada ya mazishi kukamilika ihifadhiwe kwa ajili ya mtoto wa Masogange ambaye anatarajia kuingia kidato cha kwanza mwakani.
Hayo yamezungumzwa na msanii wa maigizo ya uchekeshaji, Steve Nyerere pindi alipohojiwa na moja ya chombo cha habari hapa nchini.
Steve amesena uamuzi huo ni kufuatia na ndugu wa marehemu kudai kiasi cha fedha kilichobakia katika msiba wa ndugu yao Agness Gerard aliyefariki dunia Aprili 20, 2018 katika hospitali ya Mama Ngoma ambako alilazwa kwa kusumbuliwa na ugonjwa wa Pumu.
-
Nicki Minaj afichua siri, aitangaza tarehe yake
-
Harmonize ‘kulizwa’ na Mwarabu Fighter ilivyonikumbusha ya Jay Z, Bey
-
Mfanyabiashara amdai Ali Kiba matunzo ya mtoto Mahakamani
Steve Nyerere amesema kiasi cha fedha kilichobakia mpaka sasa mara baada ya kumaliza shughuli yote ya kumpumzisha marehemu Masogange ni shilingi Milioni mbili ambazo zimehifadhiwa benki kwa ajili ya mtoto wa Masogange.
Steve amesema kuwa kwa mazingira walioona sio rahisi ndugu kumkabidhi kiasi hiko cha fedha mtoto huyo hivyo wameaamua kumuhifadhia mpaka pale atakapoanza elimu ya Sekondari mwakani.
Aidha amesema ameshangazwa na familia hiyo kuomba kiasi cha fedha kilichobakia baada ya kutumia nafasi hiyo kutoa shukrani kwa wasanii wa filamu nchini kwa ushirikiano waliouonesha wakubeba msiba mzima na kuhakikisha ndugu yao anapumzika kwa amani.
”Mimi nilidhani familia inasimama inasema tuchukue nafasi hii kuwashukuru wasanii wote waliochanga, waulize hela iliyotumika kubeba maiti wanjua, costa mbili zilizotumika hapa hadi Mbeya Wanajua, leaders kukodi pale wanajua, Agnes tulimsaidia kwa sababu ndani ya bongo movie marehemu alikuwa rafiki yetu alikuwa najitoa, amesema Steven Nyerere”.