Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Damas Ndumbaro ameahidi kulishugulikia suala la ongezeko la makazi ya watu katika hifadhi ya Ngorongoro, kutoka watu 9000 hadi takribani watu 100,000 kiasi ambacho kinaweza kupelekea kupungua kwa wanyama katika hifadhi hiyo.
Akizungumza na Dar24, Ndumbaro amesema Wizara hiyo itakaa na wadau, Mbunge wa Ngorongoro pamoja na wananchi wa eneo hilo kufanya tathmini ya kina na kuwasilisha tathmini yao kwa Rais ili hatua zingine ziweze kufuatwa.
“Namba huwa hazidanganyi tayari hapo kuna tatizo bayana kabisa” Amesema Waziri Ndumbaro.
Aidha, akizungumzia kuhusu ukusanyaji wa maduhuli Waziri Ndumbaro amesema ni suala ambalo atalitilia mkazo.
Hata hivyo Ndumbaro amewashauri waajiriwa serikalini kufanya kazi kwa bidii kwa kuchapa kazi, kuwa waadilifu, kuacha rushwa pamoja na kuheshimu na kutekeleza maagizo ya viongozi.