Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya Darasa la Nne na Kidato cha Pili kwa watahiniwa wa mwaka 2022, huku ufaulu ukishuka kwa asilimia 82.95 kwa darasa la nne na kidato cha pili kwa asilimia 85.18 ukilinganisha na mwaka uliopita

Matokeo hayo yametangazwa leo Januari 4, 2023 na Katibu Mtendaji wa NECTA, Athumani Amasi wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema amesema ufaulu umeshuka ikilinganishwa na mwaka 2021 ambapo darasa la nne ufaulu ni asilimia 82.95 ikilinganishwa na asilimia 86.30 mwaka 2021.

Aidha, ameeleza kuwa kwa upande wa kidato cha pili ufaulu ni asilimia 85.18 ikilinganishwa na mwaka 2021 ambapo ufaulu ulikuwa asilimia 92.32.

Amasi, amesema baraza hilo limezuia matokeo ya wanafunzi 442 wa darasa la nne na wanafunzi 258 wa kidato cha pili waliopata matatizo na kushindwa kukamilisha mtihani wa upimaji wa kitaifa.

Aidha, limezuia matokeo ya wanafunzi 213 wa darasa la nne na wanafunzi 52 wa kidato cha pili ambao walibainika kufanya udanganyifu na kuvifungia vituo viwili kati ya vituo 18,645 vya mitihani vilivyothibitika kupanga na kufanya udanganyifu.

Waliofutiwa matokea wafaulu kwa asilimia 96.1
Tambwe mambo magumu Singida Big Stars