Ni Dhahir Mshambuliaji kutoka nchini Burundi Ammis Josline Tambwe ataondoka Singida Big Stars katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo la usajili.

Dalili za kuondoka kwa Mshambuliaji huyo aliyewahi kuwika akiwa na Klabu za Simba SC na Young Africans zimeonekana kufuatia namba ya jezi yake kukabidhiwa kwa Mshambuliaji Mpya wa Singida Big Stars, Francy Kasedu Kazadi.

Kazadi ameonekana akiwa na Jezi yenye namba iliyozoeleka kutumiwa na Tambwe, katika mazoezi ya Klabu ya Singida Big Stars huko Kisiwani Unguja ambako wanashiriki Michuano ya Kombe la Mapinduzi 2023.

Hata hivyo inaelezwa kuwa Tambwe ambaye aliibuka kuwa Mfungaji bora wa Ligi Daraja la Kwanza (Championship) msimu uliopita 2021-2022, yupo mbioni kutolewa kwa Mkopo ama kama itashindikana basi atachwa moja kwa moja.

Tangu kupanda Daraja kwa Klabu hiyo ya Mkoani Singida ikitokea Ligi Daraja la Kwanza (Championship), Tambwe amekuwa katika wakati mgumu wa kupata nafasi ya moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza cha Singida Big Stars chini ya Kocha Mkuu kutoka nchini Uholanzi Hans Van Der Pluijm.

NECTA: Ufaulu kidato cha pili, darasa la nne washuka
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Januari 4, 2023