Klabu ya Newcastle United imeripotiwa kupanga kutumia Pauni Milioni 150 katika dirisha lijalo la usajili, huku beki wa kushoto wa Arsenal, Kieran Tierney na winga wa Bayer 04 Leverkusen, Moussa Diaby wakiwa kwenye orodha yao.

Tierney mwenye umri wa miaka 25, ni mchezaji wa kimataifa wa Scotland akiwa na mechi 37 za wakubwa kwa jina lake, lakini licha ya kucheza mechi 22 za Ligi Kuu msimu huu, ameanza michezo mitano tu.

Kocha wa Newcastle, Eddie Howe, ana nia ya kumrejesha Dan Burn katika eneo la ulinzi la kati na anamwona Tierney kuwa na uwezo wa kuchukua nafasi muhimu zaidi ya aliyo nayo pale Arsenal kwa sasa.

Wakati huo huo, winga wa Leverkusen, Diaby, mwenye umri wa miaka 23, ndiye anayepewa kipaumbele katika safu ya tatu ya mbele, akiwa amechangia mabao 14 na asisti 10 kwenye mechi zake 41 katika mashindano yote msimu huu.

Kwa mujibu wa The Sun, Howe ameambiwa atapewa pauni milioni 150 za kutumia, na anaamini pauni milioni 30 ni bei nzuri kwa Tierney kama beki wake mpya wa kush- oto anayetarajiwa.

Diaby pia anahitajika na timu kadhaa, wakiwamo washindani wao wa Ligi Kuu, Arsenal na anatarajiwa kugharimu karibu pauni milioni 62.

Newcastle pia wanaripotiwa kumtaka mchezaji mwenza wa Diaby pale Leverkusen, Mitchel Bakker, ambaye ni beki wa kushoto mwenye umri wa miaka 23.

Watanzania waliokwama Sudan wawasili nchini salama
Redouane Jiyed kupuliza kipyenga Jumapili Kwa Mkapa