Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2022, Wilayani Ngara, zimeanza kwa ukaguzi, kuweka jiwe la msingi na kuzindua Miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 3, yenye thamani na manufaa kwa Taifa na wananchi kiujumla.

Akizungumza katika eneo hilo, Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru, Sahili Geraruma ameupongeza uongozi wa Halmashauri kwa usimamizi mzuri wa mradi na kuwasisitiza wataalam wa Halmashauri kusimamia miradi, kutunza nyaraka, kuzingatia vipimo vilivyoelekezwa na Wizara na kufuata taratibu zote za manunuzi.

Maelekezo juu ya miradi inayotekelezwa na kusimamiwa na Serikali Mkoani Kagera.

Amesema, “Vyumba vya madarasa nane vilivyojengwa kwa fedha za Uviko-19 na viwili kwa fedha za tozo, katika ukaguzi uliofanywa na Mwenge wa Uhuru kwa madarasa yote kumi mradi ni mzuri, pongezi kwa wote waliosimamia mradi huu.”

Akiwa katika mradi wa maji wa Rusumo, ambao chanzo chake ni mto Ruvuvu unaofadhiliwa na Bank ya Dunia WB, Geraruma amesema mradi huo utakapokamilika utawakomboa wananchi na kusisitiza ujengwe kwa kasi ili uweze kukamilika kwa wakati.

Mwenge pia ukazindua Miradi mbalimbali ya kimaendeleo Wilayani Ngara, Mkoani Kagera.

Katika hatua nyingine, Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge amegawa vyandarua kwa akina mama wajazito katika kundeleza kampeni ya mapambano dhidi ya Malaria, kugawa kadi za bima ya Afya iliyoboreshwa, na kuzindua klabu ya Wapinga Rushwa na Mapambano dhidi ya madawa ya Kulevya, katika shule ya Sekondari Rusumo.

Mwenge huo, ulioanza mbio zake Oktoba 07, 2022 Wilayani Ngara umekagua Mradi wa Vijana, Kikundi cha Tehama (RUDII), kilichopewa mkopo wa Halmashauri Sh. milioni 14, kuweka jiwe la msingi Mradi wa Maji Rusumo wenye thamani ya Sh. bilioni 2.7 na kuzindua barabara ya lami (km 0.6), Nakatunga-Onesmo Mikate wenye thamani ya Sh. milioni 238.1.

Mwenge wa Uhuru, Wilayani Ngara – Kagera.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Octoba 08, 2022  
Pamba yapigiwa chapuo biashara Kimataifa