Zao la Pamba limeainishwa kuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo ya jamii na uchumi wa mataifa mbalimbali duniani, hivyo kupigiwa chapuo ya kuchukua hatua madhubuti, kuhakikisha zao hilo linaendelezwa na wakulima wake kulindwa dhidi ya changamoto mbalimbali zikiwemo mabadiliko ya tabianchi.

Wito huo umetolewa na Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO, kupitia taarifa maalumu iliyotolewa hii leo Oktoba 7, 2022 mjini Roma Italia, katika kuadhimisha siku ya pamba duniani, huku ikiongeza kuwa inakadiriwa wakulima wa familia milioni 100 katika nchi 80 wanategemea sekta ya pamba, na wanawake wana jukumu muhimu katika mnyororo wa thamani wa zao hilo.

Kwa mujibu wa FAO, pamba inasaidia uchumi wa nchi nyingihususani zenye kipato cha chini na zinazoinukia na kwa mwaka wa 2021, uzalishaji wa zao hilo ulimwenguni ulikadiriwa kuwa karibu dola bilioni 50, wakati biashara ya kimataifa ilikuwa dola bilioni 20.

Uuzaji wa Pamba sokoni.

Mkurugenzi wa idara ya masoko na biashara katika shirika la FAO, Boubaker Ben Belhassen anasema “Pamba ina mchango mkubwa katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi, biashara ya kimataifa na kupunguza umaskini na hivyo kuchangia katika kufikiwa kwa ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu na malengo ya maendeleo endelevu SDG’s.”

Hata hivyo, sekta hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi kutokana na mabadiliko ya tabianchi, wadudu waharibifu na magonjwa, janga la Uviko-19 na kudorora kwa uchumi wa dunia, sambamba na masuala mengine, huku kuyumba kwa bei ya soko kukiathiri sekta hiyo kwa sehemu kubwa Duniani.

Ngara yapongezwa usimamizi miradi ya maendeleo
Sera kusaidia utambuzi uhalifu wa kupangwa, ugaidi