Msanii wa maigizo ya vichekesho hapa nchini Steve Nyerere ametaka kutokuchonganishwa na msanii wa bongo fleva hapa nchini Omary Nyembo au Ommy Dimpoz kufuatia kauli yake aliyoitoa kipindi msanii huyo amepata matatizo yaliyopelekea kufanyiwa upasuaji mkubwa kwenye koo na kupoteza sauti yake.
Mbali na hilo Steve amemuomba radhi Ommy pamoja na watanzania kwa ujumla kwa kutoa kauli yenye kumdidimiza msanii huyo aliyepata umaarufu na anayeendesha maisha yake kupitia sauti yake anayoitumia kufanya muziki mzuri unaopendwa na watu wengi.
Mara baada ya Ommy kufanyiwa upasuaji kwenye koo la chakula baada ya madaktari kubaini alikula/kunywa chakula chenye sumu, sauti ya Ommy haikuweza kutoka kwa mshindo mkubwa hali iliyopelekea Steve Nyerere kutoa matamko kuwa Omy hatoweza kuimba tena.
-
Wasafirishaji wa Mirungi wageuka kuwa Wanafunzi
-
Mwanafunzi darasa la tatu ajinyonga kwa shati la shule
‘’Kwanza nichukue fursa hii kumshukuru M/Mungu lakini nichukue fursa hii kumuomba radhi nduf yangu Dimpoz kwa namna alivyopokea kauli yangu niliyoitoa dhidi yake, Na zaidi niwaombe radhi watanzania wote na wapenzi wa sanaa’’
’Binadamu unapoona hapa umekosea busara inatutaka kukiri kukosea name nakiri kutokana na ile kauli yangu kwa Dimpoz’’ amesema Steve.
Ujio wa ngoma mpya ya Ommy inayoenda kwa jina la ‘Ni wewe’ ulimuinamisha kichwa chini Sreve Nyerere na kumfanya akiri kutoa matamko hayo yaliyokinzana na nguvu ya Mungu.
Aidha Ommy ameridhia msamaha ulioombwa na Steve na kusema kuwa hayo tayari yalitokea na yaachwe yapite ili kuruhusu maisha kuendelea, Zaidi ameshukuru kwa msanii huyo kumpa sapoti ya kuuposti wimbo wake.