NightClub moja ya Toronto, Canada ambayo rapper Drake Dreezy alikuwa akihost tukio la burudani jana usiku ilivamiwa na watu waliojihami kwa silaha za moto waliowafyatua risasi na kusabibisha vifo vya watu wawili.

Mkuu wa polisi msaidizi wa Toronto, Peter Sloly alisema kuwa tukio hilo lilitokea ndani ya club hiyo katika eneo la maonesho, Jumanne majira ya saa tisa usiku ingawa kulikuwa na polisi wengi nje ya ukumbi huo.

Alieleza kuwa mashambulizi hayo yalianzia ndani ambapo mtu mmoja alipigwa risasi kisha kuhamia nje ambapo mtu mwingine pia alipigwa risasi. Watu watatu walijeruhiwa kutokana na shambulioa hilo.

eneo la tukio

Uongozi wa club hiyo ulitoa tamko kuwa walikuwa wameweka ulinzi wa kutosha wa zaidi ya watu 70 lakini pia upekuzi wa kieletroniki ulifanyika hivyo haikufanya uzembe wowote.

Hata hivyo, polisi hawakuweka wazi kama Drake alikuwa bado ndani ya eneo la tukio wakati huo pamoja na timu yake.

Vituko Kati Ya Mourinho Na Wenger Vyaendelea
Daktari Wa Aspetar Afichua Siri Ya Di Maria Na PSG