Kitendawili cha kwanini kiongozi wa Nako 2 Nako, Lord Eyez hasikiki na haonekani kati ya wale members wa kundi la Weusi hivi sasa kimeteguliwa na msemaji wa kundi hilo, Nikki wa Pili.

Nikki ameeleza kuwa wamefanya jitihada zote za kuhakikisha rapa huyo anafanya kazi na kundi hilo na kumfungulia milango yote lakini jitihada hizo zimeshindikana.

Sababu za kugonga mwamba kwa jitihada hizo ni rapa huyo kutoonekana katika meza ya mapishi ya mashairi ya Weusi.

“Kwa sababu haingii ofisini, kwa sababu… kwa mfano hapa [studio] si ni ofisini? Mtu asipokuja ofisini najua hataweza kuonekana kwenye kazi ya Millard Ayo Production. Kwa hiyo hiyo ndio sababu, hajaingia ofisini [ndio maana haonekani kwenye kazi za Weusi],” Nikki aliiambia ‘Amplifaya’ ya Clouds Fm.

Hata hivyo, Nikki wa Pili alieleza kuwa rapa huyo aliwaambia kuwa anahitaji muda wa kupumzika jijini Arusha na kwamba sababu za kuchukua uamuzi huo anazijua yeye mwenyewe.

“Explanation ya Lord Eyez sasa hivi inabidi yeye mwenyewe ndiye atoe, sisi hatuna explanation tena. Hakuna tatizo lolote… kuna vitu vingi of course siwezi kusema hapa lakini nafikiri mazingira yalishawekwa vizuri sana na kwa nguvu zote kwa ajili yake,” aliongeza.

 

Unaweza Kuigiza Kama Sokwe? Unatafutwa Kwa Filamu Hii Ya Kimataifa
Hali Si Shwari Katika Riadha Kenya