Waandaji wa filamu zilizoishika dunia ya wapenda filamu, 20th Century Fox wamenzisha shindano la kumtafuta mhusika atakayeweza kuigiza kama Sokwe kwenye toleo jipya la filamu kubwa ya ‘Planet of The Apes’.

Muigizaji huyo atapata nafasi ya kuigiza na nyota mashuhuri wa filamu duniani, Andy Serkis ambapo toleo jipya la filamu hiyo limepewa jina la ‘War of The Planet of the Apes’ na inatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwaka 2017.

Mshiriki anaependa kuigiza katika filamu hiyo anapaswa kurekodi video fupi akiwa anaikiza kama Sokwe na kuituma kwa waandalizi wa filamu hiyo kupitia tovuti ya www.apescontest.com .

Muigizaji huyo anatafutwa ili awe miongoni mwa Sokwe watakaokuwa kwenye himaya ya Serkis ambaye ataendelea kuigiza kama mwanzilishi wa himaya ya Sokwe.

Filamu hiyo itakuwa ya tatu kwenye mfululizo wa filamu hizo, ya kwanza ikiwa Rise of the Planet of the Apes na ya pili Dawn of the Planet of the Apes ambayo ilitolewa mwaka uliopita.

 

Waziri Mkuu aanza na Mkwamo wa Mabasi ya Mwendo Kasi, atoa Saa chache kupewa majibu
Nikki Wa Pili: Lord Eyez Hafiki Ofisini Ndio Sababu Haonekani Kwenye Kazi Za Weusi