Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Nickson Simon ‘Nikki wa Pili’ amefunguka vipaumbele vyake baada ya kuapishwa na Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge kuwa Mkuu wa wilaya hiyo.
Amesema hayo mara baada ya kuapishwa rasmi kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe ambapo amesema tutashirikiana na wakuu wengine wa wilaya lengo likiwa ni kuleta maendeleo kwa watanzania wanaowatumikia.
”Tutaanza kutatua kero za wananchi hasa kero zamogogoro ya ardhi kila mmoja anapaswa kuibunka na vipaumbele vya wilaya yake baada ya muda namimi ntakuja na vipaumbele vya wilaya yangu lakini tuko hapa kutekeleza ilani ya chama ambayo lengo lake ni moja tu kuwaletea maendeleo wananchi, mwanzo wakazi tutaanza na hayo maelekezo ambayo ameyatoa mkuu wa mkoa” amesema Nikki wa Pili .
Pia ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram “Kwanza namshukuru Mungu, pili Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kuniamini na kunipa nafasi ya kuwatumikia wananchi wa Kisarawe na Serikali”
“Nina ahidi kutumia vipawa vyangu, busara zangu na uwezo wangu kuifanya kazi hii nikishirikiana na watumishi wenzangu pamoja na wananchi kusukuma mbele gurudumu la maendeleo. Shukrani kwa wote walio nitumia salamu za pongezi na mimi nawasalimu kwa jina la Jamuhuri ya Muungano” ameandika Nikki wa Pili