Mbunge wa Jimbo la Bunda, Ester Bulaya ambaye pia ni Waziri Kivuli, wa Sera Bunge Kazi, Vijana na Ajira ameibuka na kulalamikia juu ya sheria mpya ya mifuko ya hifadhi ya jamii ya mwaka 2017 ambayo iliwasilishwa bungeni hivi karibuni na kujadiliwa na wabunge.

Mbunge huyo amesema kuwa, aliamua kukaa kimya katika kipindi cha miaka mitatu ili kujua ni kwa jinsi gani serikali ya awamu ya tano inafanya kazi katika wizara ambayo yeye kama Waziiri Kivuli anaihudumia.

“Niliamua kutozungumza chochote kama Waziri kivuli wa Sera Bunge Kazi, Vijana na ajira kwa kipindi cha miaka 3 nione mwenendo wa serikali ya awamu ya tano inafanya nini, kuhusu wafanyakazi, vijana na bunge,tuliwaambia dhamira ya kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii ilikuwa ni serikali kukwepa madeni inayodaiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo kwa sasa inafikia trilioni 8 kwa sababu waliwekeza kwenye miradi isiyokua na tija,”amesema Bulaya

Hata hivyo, Mbunge huyo alikuwa ni miongoni mwa wabunge ambao walikuwa wakitajwa huenda wakajiunga na Chama Cha Mapinduzi kufuatia kuwepo kwa wimbi kubwa la waliokuwa wabunge wa upinzani kuhama vyama vyao kwa sababu mbalimbali ambapo kwa sasa ndiyo mara ya kwanza ameibuka na kuzungumza kwa umma.

 

JPM afanya uteuzi mwingine
Jaji Mkuu wa Marekani amvaa Rais Trump, adai hakuna jaji wa Obama