Nahodha wa timu ya taifa ya Rwanda, Haruna Niyonzima ameingia kwenye kumbukumbu za FIFA baada ya kuinga kwenye “FIFA’s Century Club” amabayo inawahusisha wachezaji waliocheza michezo 100 ya timu za taifa.
Niyonzima alianza kuichezea timu yake ya taifa ya wakubwa mwaka 2006 na amefanikiwa kucheza michezo 104 na kufunga magoli 6 na kuwa mchezaji pekee aliyecheza michezo mingi kwenye timu ya taifa ya Rwanda.
Wachezaji ambao wanaingia kwenye FIFA’s Century Club ni wachezaji waliocheza michezo ya kombe la dunia, hatua ya mtoano, michezo ya kufuzu, kombe la mabara na fainali za Olimpiki kuanzia mwaka 1948 kwa waliocheza timu za wakubwa tu.
Mpaka tarehe 16 Oktoba 2021 ni wachezaji 575 ambao wamefikisha michezo 100 ya huku kimataifa wakiwa na timu zao kulingana na nakala iliyotolewa na FIFA ya, Rec. Sport Soccer Statistics Foundation (RSSSF).
Katika jarida la RSSSF linamtambua Billy Wright kuwa ndie mchezaji wa kwanza kufikisha michezo 100 ya kimataifa akiwa na timu ya Uingereza mwaka 1959 akimaliza na michezo 105 wakati mchezaji aliyecheza michezo mingi ni s Bader Al-Mutawa wa kuwait akiwa na michezo 186.
Credit – Global