Msanii wa Bongo Fleva, Nuh mziwanda amesema kuwa pamoja na mitiani ya maisha anayo pitia hivi sasa bado hajakata tamaa na muziki anaoufanya.

Nuh Mziwanda ambaye hivi karibuni ndoa yake ikivunjika ndani ya muda mfupi na mkwewe kuolewa na mtu mwingine, amesema anawashukuru sana mashabiki wake kwani wamekuwa wakimfariji pindi anapopata matatizo.

Msanii huyo amesema amekuwa akipokea jumbe nyingi za mashabiki kupitia mitandao ya kijamiii wakimpa pole na kumsihi asiache muziki. Hivyo, wamesaidia kuzika mpango wa kuachana na muziki.

“Mimi siwezi kuacha muziki. Nitaendelea kufanya muziki na mashabiki wangu wana huruma sana pindi nipatapo matatizo, wananitumia ujumbe kwenye mitandao. DM huwa inajaa Messages (jumbe) nyingi. Napokea pole nyingi na wananifariji sana,” Nuh ameiambia E-News ya EATV.

Hivi karibuni, Nuh ameachia wimbo wake mpya ‘Bao la Ushindi’ ambao umetayarishwa kupitia studio anayoimiliki ya ‘Last Born Records’.

Wekeni vipaumbele vya kuendeleza viwanda nchini- Samia Suluhu
Matonya awavaa WCB, adai wamemuibia ‘Zilipendwa’