Kocha wa timu ya taifa ya Hispania Julen Lopetegui ametangaza majina ya wachezaji 23 watakaounda kikosi kitakachoshiriki michuano ya kombe la dunia nchini Urusi huku majina ya wachezaji nyota kama Alvaro Morata, Cesc Fabregas na Marcos Alonso yakikosekana katika kikosi hicho.
Nyota wengine walioachwa katika kikosi hicho ni pamoja na kiungo wa klabu ya Manchester United Ander Herrera pamoja na beki wa Arsenal Hecter Bellerin.
Wachezaji wanaocheza ligi kuu ya Uingereza walioitwa katika kikosi hicho ni pamoja na golikipa David de Gea wa Man Utd,Cesar Azpilicueta wa Chelsea,Nacho Monreal wa Arsenal na David Silva kutoka Man City.
Majina mengine yaliyotajwa ni Pepe Reina na Kepa Arrizabalaga upande wa walinda mlango.
Mabeki ni Dani Calvajal,Avro Odriozola,Gerald Pique, Sergio Ramos na Jordi Alba wakati upande wa viungo ni Sergio Busquets, Saul, Koke, Thiago Alcantala na Andres Iniesta.
Morata ambaye wengi walitegemea angeitwa katika safu ya ushambiliaji ameachwa na washambuliaji walioitwa katika kikosi hicho ni Diego Costa,Iago Aspas, Rodrigo, Marco Asensio, Lucas Vazquez na Isco.