Kiongozi wa Muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya (NASA), Raila Odinga amesema kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Tume Huru wa Uchaguzi na Mipaka (IEBC) nchini humo Ezra Chiloba bado yupo ofisini ingawa alisema kuwa amechukua likizo na asingeshiriki katika uchaguzi.
Ameyasema hayo katika mkutano wa kampeni za uchaguzi wa marudio huko Keroka, kata ya Kisii, ambapo amesema kuwa Chiloba amekwenda katika Ofisi hiyo asubuhi ya jana na kwamba anaendelea na shughuli zake za tume kama kawaida.
“Nataka niwahakikishie kuwa Afisa mtendaji mkuu wa tume bado anaendelea na majukumu yake kama kawaida licha ya kusema kuwa anachukua likizo ya wiki tatu, Chiloba hajaenda likizo,”amesema Odinga
Hata hivyo, Kenya inatarajiwa kufanya uchaguzi wa Marudio Oktoba 26 siku ya Alhamisi baada ya ule uchaguzi mkuu uliofanyika Agust 08 kufutwa na Mahakama ya juu nchini humo kwa madai kuwa kulikuwa na dosari.
-
Trump kuamuru siri ya mauaji ya ‘Rais Kennedy’ kuwekwa hadharani
-
Uteuzi wa Mugabe kuwa balozi wa ‘WHO’ waibua maswali
-
Mugabe aitikisa WHO, yafikiria upya uamuzi wake