Kiongozi wa ACT- Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema kuwa yupo tayari kuwajibika kwa kile kinachodaiwa kupika taarifa za serikali endapo Rais Dkt. Magufuli ataruhusu ukaguzi maalumu wa CAG kwenye mapato ya mwezi Julai na Agosti mwaka huu.

Amesema kuwa wao wanatumia takwimu za serikali kuwaonyesha wananchi kuwa serikali yao inadanganya na haisemi ukweli wote na uhalisia wa uchumi na kuporomoka kwa mapato.

Aidha, amesema kodi inayokusanywa na TRA nchini inaweza kulipa mishahara na kuhudumia deni la Taifa tu na si vinginevyo kama inavyoelezwa sehemu mbalimbali kuhusiana na suala la kukua kwa uchumi.

Hata hivyo, katika taarifa yake aliyitoa katika mitandao yake ya kijamii, amesema kuwa taarifa kamili kuhusu kupikwa kwa taarifa za serikali, ztatolewa mara baada ya kamati kuu ya chama cha ACT- Wazalendo.

Florentino Perez amgwaya Harry Kane
Odinga amkomalia Afisa wa IEBC