Kiongozi wa Mmuungano wa Azimio la Umoja Kenya, Raila Odinga amepinga mapendekezo yaliyo katika umswada unaopendekezwa wa ukusanyaji ushuru nchini humo akisema unafaa kuangaliwa upya kutokana na mambo mengi kutowekwa wazi kwa wakenya.
Akizungumza jijini Nairobi na kupitia andiko lake la Twitter, Odinga amesema atapinga mswada huo kutokana na mzigo wa ushuru ambao utaelekezwa kwa Wakenya iwapo utaidhinisha kwani pendekezo la kutozwa asilimia 3 ya mshahara kwa wafanyakazi wa umma kwa ajili ya kuwapa nyumba za bei nafuu.
Aidha, Odinga pia amepinga pendekezo la kuwatoza ushuru wa asilimia 15 kwa watu wanaojihusisha na video kwenye mitandao ya kidijitali na kuongeza kuwa matukio hayo ni njama ya Serikali kukopa fedha kwa wakenya bila ya kutaka kulipa riba kwa mikopo hiyo..
Kuhusu mazungumzo ya pande mbili kati ya serikali na upinzani, Odinga amesema upande wa Serikali umeonesha kutokua na umakini katika mazungumzo hayo, na kwamba iwapo mazungumzo hayo hayatafanyika hivi karibuni basi watatafuta namna nyingine za kushinikiza mabadiliko.