Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR, imesema Serikali ya nchi ya Saudi Arabia, lazima isitishe sheria ya hukumu ya kifo kwa makosa yanayohusiana na dawa za kulevya.
Hatua ya OHCR inatokana na Taifa hilo la Mashariki ya Kati kuanza tena kutoa adhabu ya kifo kwa uhalifu unaohusiana na dawa za kulevya, ikiwa ni moja ya hatua inazodaio zitakomesha biashara hiyo.
Msemaji wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, Liz Throssell amesema mauaji yamekuwa yakifanyika karibu kila siku katika wiki mbili zilizopita, kufuatia kumalizika rasmi kwa muda wa kwa kusitishwa unyongaji wa miezi 21.
Tangu Novemba 10, 2022 Saudi Arabia imewanyonga wanaume 17 kwa kile kinachoitwa makosa ya dawa za kulevya na magendo, huku watatu wakitarajiwa kunyongwa Jumatatu ambapo walionyongwa hadi sasa ni Wasyria wanne, Wapakistani watatu, Wajordani watatu na Wasaudi saba.